Lithuanian

Swahili: New Testament

Ephesians

3

1Todėl aš, Paulius, esu Kristaus Jėzaus kalinys dėl jūsų­ pagonių.
1Kutokana na hayo, mimi Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu, namwomba Mungu.
2Jūs esate girdėję apie Dievo malonės tvarkymą, man suteiktą jūsų labui.
2Bila shaka mmekwisha sikia kwamba Mungu, kwa neema yake, alinikabidhi kazi hii niifanye kwa faida yenu.
3Apreiškimu man buvo atskleista paslaptis, kaip aš ką tik trumpai aprašiau.
3Mimi nilijulishwa kwa njia ya ufunuo mpango wake uliofichika. (Nimeandika kwa ufupi juu ya jambo hili,
4Skaitydami galite įsitikinti, kad suvokiu Kristaus paslaptį,
4nanyi mkiyasoma maneno yangu mtaweza kujua jinsi ninavyoielewa siri hiyo ya Kristo.)
5kuri ankstesnėms žmonių kartoms nebuvo paskelbta taip, kaip ji dabar Dvasios atskleista Jo šventiesiems apaštalams ir pranašams:
5Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho.
6pagonys yra bendrapaveldėtojai, priklauso vienam kūnui ir yra pažado dalininkai Kristuje per Evangeliją,
6Siri yenyewe ni hii: kwa njia ya Habari Njema watu wa mataifa mengine wanapata sehemu yao pamoja na Wayahudi katika zile baraka za Mungu; wao ni viungo vya mwili uleule, na wanashiriki ahadi ileile aliyofanya Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.
7kurios tarnu tapau pagal Dievo malonės dovaną, kuri man buvo duota Jo jėgos veikimu.
7Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Habari Njema kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.
8Man, visų šventųjų mažiausiajam, atiteko malonė skelbti pagonims nesuvokiamus Kristaus turtus
8Mimi ni mdogo kuliko watu wote wa Mungu; lakini amenijalia neema yake, ili niwahubirie watu wa mataifa utajiri wake Kristo usiopimika,
9ir atskleisti visiems, kaip turi išsipildyti šita paslaptis, nuo amžių uždengta Dieve­viską sukūrusiame per Jėzų Kristų,­
9tena niwaangazie watu wote waone jinsi mpango wa Mungu uliofichika unavyotekelezwa. Mungu aliye Muumba wa vitu vyote alificha siri hiyo yake tangu milele,
10kad dabar per bažnyčią taptų žinoma kunigaikštystėms ir valdžioms danguje visokeriopa Dievo išmintis.
10kusudi, sasa kwa njia ya kanisa, wakuu na wenye enzi wa mbinguni wapate kuitambua hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi.
11Tai atitinka amžinąjį nutarimą, padarytą Kristuje Jėzuje, mūsų Viešpatyje,
11Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
12kuriame mes turime drąsą ir užtikrintą priėjimą per tikėjimą Juo.
12Basi, katika kuungana na Kristo, na kwa njia ya imani katika Kristo, sisi tunathubutu kumkaribia Mungu kwa uhodari.
13Todėl prašau nenusiminti dėl mano vargų jūsų dėlei, nes jie yra jūsų šlovė.
13Kwa hiyo, nawaombeni msife moyo kwa sababu ya mateso ninayopata kwa ajili yenu, maana hayo ni kwa ajili ya utukufu wenu.
14Dėl to aš klaupiuosi prieš mūsų Viešpaties Jėzaus Kristaus Tėvą,
14Kwa sababu hiyo, nampigia magoti Baba,
15iš kurio visa šeima danguje ir žemėje turi vardą,
15aliye asili ya jamaa zote duniani na mbinguni.
16kad iš savo šlovės turtų duotų jums sustiprėti Jo jėga per Dvasią vidiniame žmoguje,
16Namwomba Mungu, kadiri ya utajiri wa utukufu wake, awajalieni kwa uwezo wa Roho wake, nguvu ya kuwa imara ndani yenu,
17kad Kristus per tikėjimą gyventų jūsų širdyse ir jūs, įsišakniję ir įsitvirtinę meilėje,
17naye Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani. Namwomba mpate kuwa na mzizi na msingi katika mapendo
18galėtumėte suvokti kartu su visais šventaisiais, koks yra plotis, ir ilgis, ir gylis, ir aukštis,
18kusudi muweze kufahamu pamoja na watu wote wa Mungu jinsi upendo wa Kristo ueneavyo kwa mapana na marefu, kwa kimo na kina.
19ir pažinti Kristaus meilę, kuri pranoksta pažinimą, kad būtumėte pripildyti visos Dievo pilnatvės.
19Naam, mpate kujua upendo wa Kristo upitao elimu yote, mjazwe kabisa utimilifu wote wa Mungu.
20O Tam, kuris savo jėga, veikiančia mumyse, gali padaryti nepalyginamai daugiau, negu mes prašome ar suprantame,
20Kwake yeye ambaye kwa nguvu yake ifanyayo kazi ndani yetu, aweza kufanya mambo makuu zaidi ya yale tuwezayo kuomba au kufikiria;
21Jam tebūna šlovė bažnyčioje Kristuje Jėzuje per visas kartas amžių amžiais! Amen.
21kwake Mungu uwe utukufu katika kanisa na katika Kristo Yesu, nyakati zote, milele na milele! Amina.