1Daugel kartų ir įvairiais būdais praeityje Dievas yra kalbėjęs tėvams per pranašus,
1Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii,
2o šiomis paskutinėmis dienomis prakalbo mums per Sūnų, kurį paskyrė visa ko paveldėtoju ir per kurį sutvėrė pasaulius.
2lakini siku hizi za mwisho, amesema nasi kwa njia ya Mwanae. Yeye ndiye ambaye kwa njia yake Mungu aliumba ulimwengu na akamteua avimiliki vitu vyote.
3Jis, Dievo šlovės spindesys ir Jo esybės tikslus atvaizdas, viską laikantis savo jėgos žodžiu, pats nuplovęs mūsų nuodėmes, atsisėdo Didybės dešinėje aukštybėse,
3Yeye ni mng'ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwapatia binadamu msamaha wa dhambi zao, aliketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.
4tapdamas tiek pranašesnis už angelus, kiek prakilnesnį už juos paveldėjo vardą.
4Mwana ni mkuu zaidi kuliko malaika, kama vile jina alilopewa na Mungu ni kuu zaidi kuliko jina lao.
5Kuriam gi angelų kada nors Jis yra pasakęs: “Tu esi mano Sūnus, šiandien pagimdžiau Tave”?! Ir vėl: “Aš Jam būsiu Tėvas, o Jis bus man Sūnus”.
5Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: "Wewe ni Mwanangu; Mimi leo nimekuwa Baba yako." Wala hakusema juu ya malaika yeyote: "Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu."
6Ir vėl, įvesdamas Pirmagimį į pasaulį, Jis sako: “Tepagarbina Jį visi Dievo angelai”.
6Lakini Mungu alipokuwa anamtuma Mwanae mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, alisema: "Malaika wote wa Mungu wanapaswa kumwabudu."
7O apie angelus sako: “Jis daro savo angelus vėjais ir savo tarnusugnies liepsnomis”.
7Lakini kuhusu malaika, Mungu alisema: "Mungu awafanya malaika wake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa ndimi za moto."
8O Sūnui: “Tavo sostas, Dieve, amžių amžiams, ir teisingumo skeptras yra tavo karalystės skeptras.
8Lakini kumhusu Mwana, Mungu alisema: "Utawala wako ee Mungu, wadumu milele na milele! Wewe wawatawala watu wako kwa haki.
9Tu pamilai teisumą ir nekentei nedorybės, todėl patepė Tave Dievas, Tavo Dievas, džiaugsmo aliejumi gausiau negu Tavo bičiulius”.
9Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Ndiyo maana Mungu, Mungu wako amekuweka wakfu na kukumiminia furaha kubwa zaidi kuliko wenzako."
10Ir: “Iš pradžių Tu, Viešpatie, padėjai pamatus žemei, ir dangūs Tavo rankų darbas.
10Pia alisema: "Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo, mbingu ni kazi ya mikono yako.
11Jie pražus, o Tu pasiliksi, jie visi sudils lyg drabužis,
11Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima, zote zitachakaa kama vazi.
12ir kaip apsiaustą Tu juos suvyniosi, ir jie bus pakeisti. Bet Tu esi tas pats, ir Tavo metai nesibaigs”.
12Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma."
13O kuriam iš angelų Jis yra kada sakęs: “Sėskis mano dešinėje, kol Aš patiesiu Tavo priešus, kaip pakojį po Tavo kojomis”?
13Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: "Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako."
14Argi jie visi nėra tarnaujančios dvasios, išsiųstos tarnauti tiems, kurie paveldės išgelbėjimą?
14Malaika ni roho tu wanaomtumikia Mungu, na Mungu huwatuma wawasaidie wale watakaopokea wokovu.