Swahili: New Testament

World English Bible

Luke

19

1Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa anapita katika njia za mji huo.
1He entered and was passing through Jericho.
2Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jina lake Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.
2There was a man named Zacchaeus. He was a chief tax collector, and he was rich.
3Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu.
3He was trying to see who Jesus was, and couldn’t because of the crowd, because he was short.
4Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo.
4He ran on ahead, and climbed up into a sycamore tree to see him, for he was to pass that way.
5Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, "Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako."
5When Jesus came to the place, he looked up and saw him, and said to him, “Zacchaeus, hurry and come down, for today I must stay at your house.”
6Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha.
6He hurried, came down, and received him joyfully.
7Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunung'unika wakisema, "Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi."
7When they saw it, they all murmured, saying, “He has gone in to lodge with a man who is a sinner.”
8Lakini Zakayo akasimama akamwambia Yesu, "Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne."
8Zacchaeus stood and said to the Lord, “Behold, Lord, half of my goods I give to the poor. If I have wrongfully exacted anything of anyone, I restore four times as much.”
9Yesu akamwambia, "Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.
9Jesus said to him, “Today, salvation has come to this house, because he also is a son of Abraham.
10Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea."
10 For the Son of Man came to seek and to save that which was lost.”
11Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. (Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, Ufalme wa Mungu ungefika.)
11As they heard these things, he went on and told a parable, because he was near Jerusalem, and they supposed that the Kingdom of God would be revealed immediately.
12Hivyo akawaambia, "Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme, halafu arudi.
12He said therefore, “A certain nobleman went into a far country to receive for himself a kingdom, and to return.
13Basi, kabla ya kuondoka aliwaita watumishi wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kila mmoja na kumwambia: Fanyeni nazo biashara mpaka nitakaporudi.
13 He called ten servants of his, and gave them ten mina coins, and told them, ‘Conduct business until I come.’
14Lakini wananchi wenzake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende wakaseme: Hatumtaki huyu atutawale.
14 But his citizens hated him, and sent an envoy after him, saying, ‘We don’t want this man to reign over us.’
15"Huyo mtu mashuhuri alirudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, na mara akaamuru wale watumishi aliowapa zile fedha waitwe ili aweze kujua kila mmoja amepata faida gani.
15 “It happened when he had come back again, having received the kingdom, that he commanded these servants, to whom he had given the money, to be called to him, that he might know what they had gained by conducting business.
16Mtumishi wa kwanza akatokea, akasema: Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara kumi ya zile fedha ulizonipa.
16 The first came before him, saying, ‘Lord, your mina has made ten more minas.’
17Naye akamwambia: Vema; wewe ni mtumishi mwema. Kwa kuwa umekuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi!
17 “He said to him, ‘Well done, you good servant! Because you were found faithful with very little, you shall have authority over ten cities.’
18Mtumishi wa pili akaja, akasema: Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara tano ya zile fedha ulizonipa.
18 “The second came, saying, ‘Your mina, Lord, has made five minas.’
19Naye akamwambia pia: Nawe utakuwa na madaraka juu ya miji mitano.
19 “So he said to him, ‘And you are to be over five cities.’
20"Mtumishi mwingine akaja, akasema: Chukua fedha yako; niliificha salama katika kitambaa,
20 Another came, saying, ‘Lord, behold, your mina, which I kept laid away in a handkerchief,
21kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukua yasiyo yako, na huchuma ambacho hukupanda.
21 for I feared you, because you are an exacting man. You take up that which you didn’t lay down, and reap that which you didn’t sow.’
22Naye akamwambia: Nakuhukumu kutokana na msemo wako, ewe mtumishi mbaya! Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, ambaye huchukua yasiyo yangu na kuchuma nisichopanda.
22 “He said to him, ‘Out of your own mouth will I judge you, you wicked servant! You knew that I am an exacting man, taking up that which I didn’t lay down, and reaping that which I didn’t sow.
23Kwa nini basi, hukuiweka fedha yangu benki, nami ningeichukua pamoja na faida baada ya kurudi kwangu?
23 Then why didn’t you deposit my money in the bank, and at my coming, I might have earned interest on it?’
24Hapo akawaambia wale waliokuwa pale: Mnyang'anyeni hizo fedha, mkampe yule aliyepata faida mara kumi.
24 He said to those who stood by, ‘Take the mina away from him, and give it to him who has the ten minas.’
25Nao wakamwambia: Lakini Mheshimiwa, huyo ana faida ya kiasi hicho mara kumi!
25 “They said to him, ‘Lord, he has ten minas!’
26Naye akawajibu: Kila aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
26 ‘For I tell you that to everyone who has, will more be given; but from him who doesn’t have, even that which he has will be taken away from him.
27Na sasa, kuhusu hao maadui wangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu."
27 But bring those enemies of mine who didn’t want me to reign over them here, and kill them before me.’”
28Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea Yerusalemu.
28Having said these things, he went on ahead, going up to Jerusalem.
29Alipokaribia kufika Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
29It happened, when he drew near to Bethsphage and Bethany, at the mountain that is called Olivet, he sent two of his disciples,
30akawaambia: "Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana punda amefungwa ambaye hajatumiwa na mtu. Mfungeni, mkamlete hapa.
30saying, “Go your way into the village on the other side, in which, as you enter, you will find a colt tied, whereon no man ever yet sat. Untie it, and bring it.
31Kama mtu akiwauliza, kwa nini mnamfungua, mwambieni, Bwana ana haja naye."
31 If anyone asks you, ‘Why are you untying it?’ say to him: ‘The Lord needs it.’”
32Basi, wakaenda, wakakuta sawa kama alivyowaambia.
32Those who were sent went away, and found things just as he had told them.
33Walipokuwa wanamfungua yule mwana punda, wenyewe wakawauliza, "Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?"
33As they were untying the colt, its owners said to them, “Why are you untying the colt?”
34Nao wakawajibu, "Bwana anamhitaji."
34They said, “The Lord needs it.”
35Basi, wakampelekea Yesu yule mwana punda. Kisha wakatandika mavazi yao juu yake wakampandisha Yesu.
35They brought it to Jesus. They threw their cloaks on the colt, and set Jesus on them.
36Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao barabarani.
36As he went, they spread their cloaks in the way.
37Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake, wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;
37As he was now getting near, at the descent of the Mount of Olives, the whole multitude of the disciples began to rejoice and praise God with a loud voice for all the mighty works which they had seen,
38wakawa wanasema: "Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana. Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!"
38saying, “Blessed is the King who comes in the name of the Lord! Peace in heaven, and glory in the highest!”
39Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwako katika lile kundi la watu, wakamwambia Yesu, "Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!"
39Some of the Pharisees from the multitude said to him, “Teacher, rebuke your disciples!”
40Yesu akawajibu, "Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaza sauti."
40He answered them, “I tell you that if these were silent, the stones would cry out.”
41Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia
41When he drew near, he saw the city and wept over it,
42akisema: "Laiti ungelijua leo hii yale yaletayo amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.
42saying, “If you, even you, had known today the things which belong to your peace! But now, they are hidden from your eyes.
43Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote.
43 For the days will come on you, when your enemies will throw up a barricade against you, surround you, hem you in on every side,
44Watakupondaponda wewe pamoja na watoto wako ndani ya kuta zako; hawatakuachia hata jiwe moja juu jingine, kwa sababu hukuutambua wakati Mungu alipokujia kukuokoa."
44 and will dash you and your children within you to the ground. They will not leave in you one stone on another, because you didn’t know the time of your visitation.”
45Kisha, Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuzia nje wafanyabiashara
45He entered into the temple, and began to drive out those who bought and sold in it,
46akisema, "Imeandikwa: Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi."
46saying to them, “It is written, ‘My house is a house of prayer,’ but you have made it a ‘den of robbers’!”
47Yesu akawa anafundisha kila siku Hekaluni. Makuhani wakuu, walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumwangamiza,
47He was teaching daily in the temple, but the chief priests and the scribes and the leading men among the people sought to destroy him.
48lakini hawakuwa na la kufanya, maana watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini kabisa.
48They couldn’t find what they might do, for all the people hung on to every word that he said.