World English Bible

Swahili: New Testament

Luke

3

1Now in the fifteenth year of the reign of Tiberius Caesar, Pontius Pilate being governor of Judea, and Herod being tetrarch of Galilee, and his brother Philip tetrarch of the region of Ituraea and Trachonitis, and Lysanias tetrarch of Abilene,
1Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, alikuwa mkuu wa mikoa ya Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
2in the high priesthood of Annas and Caiaphas, the word of God came to John, the son of Zacharias, in the wilderness.
2na Anasi na Kayafa walikuwa makuhani wakuu mjini Yerusalem. Wakati huo ndipo neno la Mungu lilipomjia Yohane, mwana wa Zakariya, kule jangwani.
3He came into all the region around the Jordan, preaching the baptism of repentance for remission of sins.
3Basi, Yohane akaenda katika sehemu zote zilizopakana na mto Yordani, akihubiri watu watubu na kubatizwa ili Mungu awaondolee dhambi.
4As it is written in the book of the words of Isaiah the prophet, “The voice of one crying in the wilderness, ‘Make ready the way of the Lord. Make his paths straight.
4Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: "Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni mapito yake.
5Every valley will be filled. Every mountain and hill will be brought low. The crooked will become straight, and the rough ways smooth.
5Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyooshwa, njia mbaya zitatengenezwa.
6All flesh will see God’s salvation.’”
6Na, watu wote watauona wokovu utokao kwa Mungu."
7He said therefore to the multitudes who went out to be baptized by him, “You offspring of vipers, who warned you to flee from the wrath to come?
7Basi, Yohane akawa anawaambia watu wengi waliofika ili awabatize: "Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mngeweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
8Bring forth therefore fruits worthy of repentance, and don’t begin to say among yourselves, ‘We have Abraham for our father;’ for I tell you that God is able to raise up children to Abraham from these stones!
8Basi, onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kusema: Sisi ni watoto wa Abrahamu. Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyageuza mawe haya yawe watoto wa Abrahamu!
9Even now the axe also lies at the root of the trees. Every tree therefore that doesn’t bring forth good fruit is cut down, and thrown into the fire.”
9Lakini, sasa hivi shoka limewekwa tayari kukata mizizi ya miti. Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni."
10The multitudes asked him, “What then must we do?”
10Umati wa watu ukamwuliza, "Tufanye nini basi?"
11He answered them, “He who has two coats, let him give to him who has none. He who has food, let him do likewise.”
11Akawajibu, "Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo."
12Tax collectors also came to be baptized, and they said to him, “Teacher, what must we do?”
12Nao watoza ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza, "Mwalimu, tufanye nini?"
13He said to them, “Collect no more than that which is appointed to you.”
13Naye akawaambia, "Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa."
14Soldiers also asked him, saying, “What about us? What must we do?” He said to them, “Extort from no one by violence, neither accuse anyone wrongfully. Be content with your wages.”
14Nao askari wakamwuliza, "Na sisi tufanye nini?" Naye akawajibu, "Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu."
15As the people were in expectation, and all men reasoned in their hearts concerning John, whether perhaps he was the Christ,
15Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusu Yohane: kuwa labda yeye ndiye Kristo.
16John answered them all, “I indeed baptize you with water, but he comes who is mightier than I, the latchet of whose sandals I am not worthy to loosen. He will baptize you in the Holy Spirit and fire,
16Hapo Yohane akawaambia wote, "Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia kamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17whose fan is in his hand, and he will thoroughly cleanse his threshing floor, and will gather the wheat into his barn; but he will burn up the chaff with unquenchable fire.”
17Yeye ni kama mtu anayeshika mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka, aipure nafaka yake, akusanye ngano ghalani mwake, na makapi ayachome kwa moto usiozimika."
18Then with many other exhortations he preached good news to the people,
18Hivyo, pamoja na mawaidha mengine mengi, Yohane aliwahimiza watu akiwahubiria Habari Njema.
19but Herod the tetrarch, being reproved by him for Herodias, his brother’s wife, and for all the evil things which Herod had done,
19Lakini Yohane alimgombeza Herode, mkuu wa mkoa, kwa sababu alikuwa amemchukua Herodia, mke wa ndugu yake, na kumfanya mke wake; na pia kwa ajili ya mabaya yote aliyokuwa amefanya.
20added this also to them all, that he shut up John in prison.
20Kisha Herode akazidisha ubaya wake kwa kumtia Yohane gerezani.
21Now it happened, when all the people were baptized, Jesus also had been baptized, and was praying. The sky was opened,
21Watu wote walipokuwa wamekwisha batizwa, Yesu naye alibatizwa. Na alipokuwa akisali, mbingu zilifunguka,
22and the Holy Spirit descended in a bodily form as a dove on him; and a voice came out of the sky, saying “You are my beloved Son. In you I am well pleased.”
22na Roho Mtakatifu akamshukia akiwa na umbo kama la njiwa. Sauti ikasikika kutoka mbinguni: "Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe."
23Jesus himself, when he began to teach, was about thirty years old, being the son (as was supposed) of Joseph, the son of Heli,
23Yesu alipoanza kazi yake hadharani, alikuwa na umri upatao miaka thelathini, na watu walidhani yeye ni mwana wa Yosefu, mwana wa Heli.
24the son of Matthat, the son of Levi, the son of Melchi, the son of Jannai, the son of Joseph,
24Heli alikuwa mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yanai, mwana wa Yosefu,
25the son of Mattathias, the son of Amos, the son of Nahum, the son of Esli, the son of Naggai,
25mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Hesli, mwana wa Nagai,
26the son of Maath, the son of Mattathias, the son of Semein, the son of Joseph, the son of Judah,
26mwana wa Maathi, mwana wa Matathia, mwana wa Shemeni, mwana wa Yoseki, mwana wa Yuda,
27the son of Joanan, the son of Rhesa, the son of Zerubbabel, the son of Shealtiel, the son of Neri,
27mwana wa Yohanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa Neri,
28the son of Melchi, the son of Addi, the son of Cosam, the son of Elmodam, the son of Er,
28mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri,
29the son of Jose, the son of Eliezer, the son of Jorim, the son of Matthat, the son of Levi,
29mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana wa Mathati, mwana wa Lawi,
30the son of Simeon, the son of Judah, the son of Joseph, the son of Jonan, the son of Eliakim,
30mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yosefu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliakimu,
31the son of Melea, the son of Menan, the son of Mattatha, the son of Nathan, the son of David,
31mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi,
32the son of Jesse, the son of Obed, the son of Boaz, the son of Salmon, the son of Nahshon,
32mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,
33the son of Amminadab, the son of Aram, the son of Hezron, the son of Perez, the son of Judah,
33mwana wa Aminadabu, mwana wa Admini, mwana wa Arni, mwana wa Hesroni, mwana wa Feresi, mwana wa Yuda,
34the son of Jacob, the son of Isaac, the son of Abraham, the son of Terah, the son of Nahor,
34mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Abrahamu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori,
35the son of Serug, the son of Reu, the son of Peleg, the son of Eber, the son of Shelah,
35mwana wa Serugi, mwana wa Reu, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala,
36the son of Cainan, the son of Arphaxad, the son of Shem, the son of Noah, the son of Lamech,
36mwana wa Kainani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Noa, mwana wa Lameki,
37the son of Methuselah, the son of Enoch, the son of Jared, the son of Mahalaleel, the son of Cainan,
37mwana wa Mathusala, mwana wa Henoki, mwana wa Yaredi, mwana wa Mahalaleli, mwana wa Kenani,
38the son of Enos, the son of Seth, the son of Adam, the son of God.
38mwana wa Enosi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, aliyekuwa wa Mungu.